HISTORIA YA DR.
LIVINGSTONE HAPA UJIJI
SAFARI ZA DR. LIVINGSTONE HUKU
AFRIKA
Dr.
David Livingstone alizaliwa huko Blantyre, Uskochi tarehe 19/03/1813. Dr.
Livingstone alisoma masomo ya udaktari wa binadamu katika chuo kikuu cha
Cambridge. Alifanya safari za kuja Afrika mara tatu kwa nyakati tofauti. Safari
yake ya kwanza alikwenda Afrika ya kusini mwaka 1841. Alikutana na Robert
Moffat ambaye alikuwa akiishi huko. Mwaka 1843 Dr. Livingstone alioa binti wa
Robert Moffat (Mary). Walifanikiwa kupata watoto watatu ambao wawili walikuwa
ni wa kiume na mmoja wa kike. Kwa bahati mbaya, ilipofika mwaka 1852 mke wa
Livingstone alifariki dunia kwa ugonjwa wa Malaria huko Chupanga, Msumbiji. Dr.
Livingstone aliwapeleka watoto wake Ulaya kwa ajili ya masomo.
Mwaka
1859, Dr. Livingstone alifanya safari yake Afrika kwa mara ya pili. Dr.
Livingstone alikuwa mzungu wa kwanza kuona maporomoko ya Victoria na mto
Zambezi katika ukanda wa Afrika ya kusini. Baada ya uvumbuzi huo, Dr.
Livingstone aliamua kurudi kwao Uingereza ili aweze kutoa hotuba yake katika
chuo kikuu cha Cambridge juu ya uvumbuzi huo. Katika hotuba yake hiyo aliwahamasisha
wazungu wenzake kuja katika bara la Afrika kufungua njia za biashara na kueneza
dini ya kikristu.
Ilikuwa
ni mwaka 1866 ambapo Dr. Livingstone alikuja Afrika kwa mara ya tatu. Lengo la
safari yake ilikuwa ni kuchunguza chanzo cha mto Nile. Safari yake ilianzia katika
chanzo cha mto Ruvuma, Mikindani Mtwara. Alifuata huu mto mpaka ziwa Nyasa,
Banguela na Mweru. Dr. Livingstone alifika mpaka kwa wamanyema (Zaire). Alikuta
biashara ya watumwa ikiwa imeshamiri sana na ilikuwa ikiendeshwa na Waarabu
pamoja na Waswahili. Dr. Livingstone alivuka maji ya ziwa Tanganyika na kufika
Ujiji kwa mara ya kwanza mwaka 1869 ambapo aliweka kambi ya muda mfupi. Mji wa Ujiji
ulipata maarufu kwa sababu ya biashara ya watumwa. Watumwa wengi walikuwa
wakikamatwa huko Zaire na Burundi na kuletwa Ujiji ili waweze kusafirishwa
kutoka Ujiji mpaka Bagamoyo. Watumwa hao walikuwa wakisafirishwa kupitia njia
ya kati ya watumwa ambayo mpaka sasa kuna ushaidi wa miti ya miembe iliyokuwa
imeoteshwa na waarabu.
HOFU YA KIFO CHA DR. LIVINGSTONE
Kwa
kipindi cha miaka mitano (1866-1871), Dr. Livingstone hukufanya mawasiliano
yoyote na serikali yake ya Uingereza. Hali hii ilizua hofu huko Ulaya kwamba huenda
Livingstone alikuwa ameshakufa huku Afrika. Katika kipindi hichi afya ya Dr.
Livingstone ilikuwa imedhoofika sana kwani alikuwa akiugua ugonjwa wa Malaria
mara kwa mara, na alikuwa akisubiri kifo chake.
UJIO WA HENRY MORTON STANLEY
Wazungu
wengi sana huko Ulaya waliamini kuwa Dr. Livingstone amekufa lakini mhariri wa
gazeti la New York Herald James Gordon Bannett (Jnr) hakuamini habari hizo za
kifo cha Dr. Livingstone. Mhariri huyu aliamua kumtuma ripota wake mahiri Henry
Morton Stanley kuja kumtafuta Dr. Livingstone huku Afrika. Stanley alikuwa
ameajiriwa huko Marekani katika gazeti la New York Herald ingawa utaifa wake
ulikuwa ni wa Uingereza.
Stanley
alifika Zanzibar tarehe 6/1/1871. Baada ya kufanya maandalizi kwa muda wa miezi
miwili ya kumtafuta Dr. Livingstone. Ilipofika mwezi wa tatu mwaka 1871 alifika
Bagamoyo.
KUKUTANA KWA STANLEY NA DR.
LIVINGSTONE CHINI YA MTI WA MWEMBE
Ilikuwa
tarehe 10/11/1871 ambapo Stanley alikutana na Dr. Livingstone kwa mara ya
kwanza hapa Ujiji. Stanley na Livingstone walikaa kwa pamoja kwa muda wa miezi
mnne katika eneo la Ujiji na Kwihara Tabora. Pia Stanley alishiriki safari za
Dr. Livingstone haswa katika ukanda wa kaskazini mwa ziwa Tanganyika. Stanley
alimshawishi Livingstone arudi kwao Uingereza lakini Dr. Livingstone alikataa.
Tarehe
14/03/1872 Stanley alikwenda pwani ya bahari ya Hindi na alifika Bagamoyo
tarehe 6/5/1872. Siku iliyofuata alikwenda Zanzibar na tarehe 19/5/1872 alifika
Uingereza. Ilipofika tarehe 1/8/1872 aliandaa hotuba mbalimbali ambazo
zimemfanya awe maarufu sana duniani hadi leo.
UMAARUFU WA MTI MKUBWA WA MWEMBE
Chini
ya mti huu wa mwembe ndipo Dr. Livingstone na Stanley walikutana kwa mara ya
kwanza hapa Ujiji. Mti huu uliishi mpaka miaka ya 1920’s. Lakini katika kipindi
hicho mti huo ulikuwa umeanza dalili za kuanza kudhoofika. Kutokana na umaarufu
wa mti huu wa mwembe, serikali ya kikoloni ya mwingereza haikutaka mti huu
upotee, ndipo ilipoamua kukata matawi manne ya mti huu na kuyapandikiza. Hivi
leo kuna miti miwili ya maembe iliyopandikizwa. Baada ya mti huu wa mwembe kufa
kuliamuriwa kujengwe mnara ili uwakilishe mti huu wenye historia ya kipekee.
Mnara huu ulijengwa mwaka 1927 chini ya serikali ya mwingereza.
KIFO CHA DR. LIVINGSTONE
Mwezi
wa nane, mwaka 1872 Livingstone alikwenda Chitambo, Zambia na alikufa huko tarehe
1/5/1873. Watumishi wake wanne Susi, Chuma, Mumwaswere na Uchopere waliufanyia
upasuaji mwili wa Livingstone na kumtolea utumbo, maini na moyo na kuviweka
katika sanduku la chuma na kulifukia chini ya mti wa Mvule. Pia waliupaka mwili
wa Livingstone chumvi na viungo vingine ili usiharibike. Walianza safari yao
kutoka Chitambo, Zambia mpaka Bagamoyo ambapo mwili wake ulipokelewa na
wamissionari. Wamissionari waliufanyia misa takatifu na kuusafirisha kwenda
Uingereza kupitia Zanzibar. Tarehe 15/4/1874 mwili wa Dr. Livingstone ulizikwa
katika makaburi ya Westminster Abbey.
MAMBO ALIYOYAFANYA DR. LIVINGSTONE
HUKU AFRIKA
i.
Dr. Livingstone alikuwa akipeleleza
Afrika juu ya tamaduni za waafrika, rasilimali zake na kuzitolea taarifa katika
taifa lake la Uingereza.
ii.
Dr. Livingstone alieneza dini ya
kikristo katika maeneo ya ndani ya Afrika.
iii. Dr. Livingstone alikomesha biashara
haramu ya watumwa. Alikuwa akinunua watumwa kwa kutumia pesa yake na kuwaachia
huru, kwani Chuma na Susi walikombolewa katika biashara hii haramu ya utumwa na
Dr. David Livingstone.
Imeandaliwa na:
Kelvin
Ngowi,
Mhifadhi
wa Mambo ya Kale,
Makumbusho
ya Dr. Livingstone,
S.
L. P. 565,
Ujiji-Kigoma, Tanzania.
0766014335,
0712207460
ngowike91@gmail.com
p
I really liked as a part of the article. With a nice and interesting topics
JibuFutastanely and livingstone
Thank you Bharath and we hope that you will visit Dr. Livingstone Museum in Ujiji Kigoma.
JibuFutaNaomba kujua mzungu alieandika mateso na madhara ya biashara ya utumwa
JibuFutaLivingstone
FutaDr Livingstone ni nani?
Dr livingstone ni mpelelezi aliye wasaidia watumwa.
FutaNimefurahi sana kupata taarifa ya Dkt.David Livingstone
JibuFutaNimevutiwa na story hii
JibuFutaNaitaji kujua ndugu zake
JibuFutaNimefurahia historia ya Dr Livingstone na huduma yake ya injili pamoja na huruma yake ya kununua watumwa na kuwaachia huru.
JibuFutaNimevutiwa na huduma ya kueneza injili ya Dr Livingstone pamoja na kuwanunua watumwa na kuwaachia huru.
JibuFuta